Je? Nimsamehe au nimlipizie Kisasi?. (Vita visivyoisha vya Afghanistan)
“.Kabla
haujaanza safari ya kwenda kulipa kisasi anza kuchimba makaburi mawili...” Confucius
(Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga).
Kisasi ni kitu kinachoweka hisia ya ahueni katika
mioyo ya binadamu kwa muda, lakini ili kikadiliwe sawasawa na mtendaji wanadamu
wamejiekea mifumo mbalimbali ya haki na hukumu ili kusuruhisha au kutoa haki
kwa jamii zao. Ili kusudi kuepusha watu kujichukulia sheria mkononi.
Lakini ndivyo ulimwengu unavyosema kuhusu kisasi ni
sehemu ya maisha ya kila jamii unapotazama maigizo, tamthiliya au kusoma riwaya
basi uwa na pande mbili zinazokinzana Mhusika mkuu na adui wa mhusika. Ambapo
kama itaanza mhusika mkuu akipitia katika mateso mikononi mwa adui zake au
jamii yake ikapitia katika mgogoro huo, basi ili tamthiliya au sinema hiyo
iishie ikiwapa tulizo na kufurahisha watazamaji sharti kisasi kilipwe au
kutokee kuingilia kati kwa Mungu au miungu kuonesha ikilipa kisasi kwa adui wa
mhusika huyo.
Hivyo
fahamu yapo mambo unaweza ukaachilia au ukayafikisha katika sehemu za sheria
ili kupatiwa haki zako (muhimu sana hili), lakini hiyo huwa haitoshi hata kama
aliyekutenda atatendwa adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi yako. lakini
usipojifunza kuachilia baada ya muda utaharibikiwa tu na wewe.
KISASI
NA MAHUSIANO YA MTENDAJI NA MTENDWA.
Baba na kijana wake mwenye tabia ya kisasi na
utukutu, baada ya kumpa adhabu mara kwa mara lakini kijana hajabadilika hivyo
akampa sehemu ya ukuta awe anaipiga na nyundo na misumali kila mara anapopatwa
na hasira ya kulipiza kwa namna zote katika kiwango ambacho wazazi na ndugu
zake watasikia milio hiyo ya upigaji.
Baada ya muda kuona haijamsaidia kuondoa hali yake
akamfuata baba yake kumuuliza. ni nini maana yake baada ya kijana kuona ukuta
kashauharibu sana ukuta ule, baba yake akamwambia “hiyo ndiyo mfano wa nafsi za
wale unaowaudhi kutokana na hasira na kupenda kulipiza kwa hata vitu visivyo na
umuhimu, ijapokuwa nduguzo huwa hawakujibu chochote kwako hivyo ndivyo jinsi
wanavyokuwa ndani ya nafsi zao”. Akaongeza na swali je? unadhani unaweza
kuurudisha ukuta kama ulivyokuwa mwanzo kabisa kwa mikono yako mwenyewe?.
CASE
STUDY: VITA ISIYOISHA YA AFGHANISTAN KWA MIONGO MINGI
“..Hao waiosamehe historia kwao hujirudia mpaka
huruma inakapochukua nafasi ya hukumu..”—Alan
Cohen
(Picha ya kielelezo inayomuonesha mwanamgambo wa Taliban amebeba
silaha aina ya RPG nchini Afghanistan).
Labda wengi wetu
tumeisikia sana Afghanistan hasa kuanzia mwaka 2001 baada ya kuangushwa kwa
majengo pacha ya biashara nchini marekani (Septemba 7) hivyo navyotamka nchini
hii kinachokuja kichwani kwako msomaji wangu ni Talibani, Osama bin laden, Mura
Omar na vita, hivi ni baadhi tu unavyovifahamu.
Lakini nakupa
elimu ya ndani kwa ufupi kuhusu kabila kubwa linaloitwa “Pashtun” ambalo lina utamaduni
wa kipekee sana na unaojulikana kama “Pashtunwali” huu ni mfumo wa kanuni
za maadili ambazo makabila mengi yamemezwa kuufuata kutokana na uwingi wa watu
wa pashtun.
Tungesema leo
hii unapotaja kanda ya ziwa kinachokuja kichwani mwa wengi ni kabila la
wasukuma lakini yapo makabila mengi madogo madogo ambayo kwa kadili muda
unavyoenda yanamezwa na utamaduni wa wasukuma. Pia Mbeya yapo makabila
madogomadogo mengi lakini yanajikuta yanaathiriwa kitamaduni na kumezwa na
kabila la Wanyakyusa.
Labda nianze leo
katika makala hii kukupa historia ya kwa ufupi kuhusu taifa la Afghanistan kwa
karne nyingi nyuma zilizopita hasa uhusiano kati ya jamii zao wenyewe pia jamii
hizo na mataifa makubwa (Super powers).
MIKONONI
MWA ALEXANDER MKUU 330 B.C ( KABLA YA KRISTO ).
Kwa mara ya kwanza Alexander the Great alifika
eneo la Afghanistan baada ya kumshinda mfalme Dario wa tatu katika pigano
liloitwa vita ya Gaugamela. Jeshi lake wakati huo akiwa ndio taifa babe
ulimwenguni lilikutana na upinzani mkali sana kutoka katika makabila ya
Afghanistan na Alexander alinukuliwa akisema hivi juu ya waafghanistani “si
ngumu kuivamia ndani kivita lakini ni vigumu kuondoka kivita”. kutoka hivyo
safari yake aikuendelea sana sababu alifariki akiwa ana miaka 30 tu. Na hivyo
utawala wake ukashindwa hapo baadaye nakuiachana nchi hiyo.
Hivyo baadaye baada ya
kuondoka kwa vikosi vyake kukapita vipindi vingi sana vya migogoro ya vita
katika ya wao kwa wao na jamii zao.
MIKONONI
MWA UINGEREZA KARNE YA 19 ( MIAKA YA 1800 ).
Katika kuelekea
karne hii ndipo mfumo wa ubepari unaanza kuchipuka ambapo taifa la uingereza
lipo katika kilele chake cha taifa babe duniani (kama ilivyo marekani leo).
iliingia Afghanistan ikitokea Pakistani (wakati huo Pakistani ilikuwa eneo la
India). Kwahiyo kuanzia mwaka 1837 ndipo uingereza ikaanza kukutana na upinzani
kutoka kwa makabila ya hapo na jeshi la uingereza likawa limeshaaithiriwa
vibaya. baadaye vikifuatiwa na vitendo vya upinzani na uasi mara kwa mara hivyo
ikabidi uingereza iitawale kwa kuirimoti (indirect rule) kutokea india.
Kuna kisa
kinachoelezewa askari wa uingereza na raia wake idadi ya watu 3000 waliamua
kuondoka kutolokea India baada ya mashambulizi ya mara kwa mara kwa watu wake.
Hivyo licha ya kukubali kuondoka waafghanistani waliendelea kuwashambulia
waingereza na msafara wao njiani kiasi inakadiliwa walioweza kuingia Pakistani hai
ni chini ya 100 tu.
Uingereza ilipoondoka nchini
humo muda si mrefu waafghanistani wakageukiana wao kwa wao tena migogoro
ikaendelea katika vipindi tofauti tofauti.
MIKONONI MWA UMOJA
WA KISOVIETI USSR (1978 MPAKA 1989).
(wanamgambo wa Mujahidina wamesimama
juu ya helikopta ya wasovieti walioitungua).
Sitaki kuelezea sana lakini kuna muda ulifika sovieti serikali yao
ilipiga marufuku jeshi lao kutumia helikopta au ndege katika anga la
Afghanistan ila mpaka kukiwa na ulazima sana kufanya hivyo kwa ajili ya kiusalama
na kwa gharama hiyo.
Sababu zilikuwa zinashambuliwa na maroketi (“RPG” angalia picha ya juu
kielelezo) mengi na kudondoshwa. Mwishoni sovieti waliamua kuondoka sababu
walishindwa vita hiyo na makabila ya waafghanistan licha ya kuwa umoja wa
kisoviet ulikuwa taifa babe sawa sawa na marekani wakati huo. Kipindi hicho
kulikuwa na kundi linaloitwa Mujahidina ambalo lilikuwa mstari wa mbele kupinga
walichoamini ni utawala wa kimabavu kwa kulinda uhuru wao na kulipiza kisasi dhidi
ya wasovieti na udhalimu wao kwa wananchi wa afghanistani.
MIKONONI MWA
KIKUNDI CHA TALIBANI.
Kundi la mujahidina likachukua utawala rasmi baada ya kumaliza uwepo wa
wasovieti nchini Afghanistan lakini
kutokana na sababu ntakazozitaja hapo baadaye kukatokea mgawanyiko ndani ya
mujahidina, wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe mwisho likazaliwa kundi la
Talibani. Kundi hili likaanza upinzani na baadaye uasi likachukua nchi mwaka
1996.
Kukawa
na utulivu mdogo wakati huo huo kukiwa na mapigano madogo madogo kati ya jamii
za pale hasa wale wenye itikadi kali na wasio na itikadi kali pia kitokana na
kanuni za sheria katika tamaduni zao ambazo wanazishika na kuzifuata sana.
MIKONONI MWA MAREKANI
( 2001 HADI 2017).
Baada ya Ndege mbili zinazosadikia kutumiwa na washirika wa Osama bin
laden kuangusha majengo pacha ya biashara nchini marekani. Marekani anaingia
rasmi katika vita na Afghanistan iliyo chini ya kundi la talibani. Kutokana na
teknolojia na ubabe kijeshi marekani anaingia ijapokuwa anapata upinzani lakini
anafanikiwa kuiangusha serikali ya kundi la Talibani. lakini licha ya nguvu za
kijeshi, kiuchumi, kitamaduni na kitekinolojia kuna wakati inaripotiwa marekani
ilikuwa inaangusha mabomu ya tani kubwa kubwa kiasi cha kufumua milima na
kuleta maangamizi makubwa na kwa mashambulizi ya silaha nzito nzito dhidi ya
watalibani ambao bado waliendelea kutoa upinzani hivyo hivyo tu kila kukicha
hawakuweka silaha zao chini.
Ni miaka mingi imepita tangia vita hiyo ianze inaenda kutimia miaka 18
huku makadilio yaliyofanywa mpaka 2017 vita imeigharimu taifa la marekani kiasi
dola bilioni 2.4 sawa na Shilingi trilioni 5,472,360,000,000,000.00 za
kitanzania.
Na hakuna matumaini ya vita kuisha ijapokuwa tayari marekani kaanza
kuyaondoa majeshi yake huku upinzani wa talibani ukiendelea kuchukua hatamu
wakiteka vijiji, miji hadi majimbo.
(Uharibifu baada ya shambulizi la
kujitoa muhanga ndani ya jengo la ibada nchini Afghanistan ).
Lakini
licha ya kuwa na serikali ya mtu wa kwao kwa sasa anaowaita wasuluhishe mezani vita
yao. Lakini jamii bado imegawanyika yapo makundi ya makabila na mabwana wa vita
ambao wanaoiunga mkono serikali yao na wale wanaoiunga mkono Talibani, ambao
wanapigana kila kukicha vijijini hadi kwenye miji.
FAHAMU KANUNI ZA
TAMADUNI ZINAZOWAONGOZA WATU WA AFGHANISTANI “PAKHTUNWALI”.
Kwa karne nyingi sana tamaduni hii ya kabila ya pashtun imeendelea
kushikiliwa na makabila ya hapo kiasi wao huiita “njia ya maisha”. Katika
tamaduni hiyo ina vitu vikuu vitatu vinavyoitwa (i).Ukarimu (mermestia), (ii).ushujaa
(tora) na (iii).kisasi (badal).
Katika jamii za wanadamu hasa wafugaji wa wanyama wale waporini au
nyumbani kifupi si kitu rahisi ukakuta simba,chui au duma ukawamuweka mmoja
wapo katika banda moja na swala au pundamilia walau hata kwa siku moja tu ni
kitu hakuna mfugaji yoyote anayeweza kukubali hilo.
Hata Mbwa tu (mfano wa kisasi) wa nyumbani
kama ukiwa haumpi matunzo mazuri halafu ukamuweka banda moja na Kuku au Sungura
(mfano wa ukarimu) lazima utakuta siku moja kawatafuna tu wote lakini kwa Paka
(mfano wa ushujaa) wataishi kwa kuogopana
na ikiwemo ugomvi mara kwa mara usioisha mpaka mmoja atakapoondoka.
Tamaduni ya kulipa kisasi kwa makabila ya Afghanistan imeenda mbali sana
kiasi kwamba unapomtukana mtu kwao utendaji haki kwa kosa hilo ni huyo
mtukanwaji kuhakikisha kamtoa damu mtukanaji (Peghor) au mtuhumiwa.
Yoyote anayevunja sheria za tamaduni yao akatoroka basi lazima kisasi kifanyike
kwa ndugu zake wa karibu kwa niaba ya mtuhumiwa hata ikiwa kwa kumwaga damu.
Hivyo kama ukitaka kupona mkimbie woote wewe na ukoo wako wote. Adhabu ya
kuuliwa ni kitu cha kawaida sana katika sheria zao, kama juzi ulimshinda vitani
Babu yao afghanistani weka akilini na
ufahamu tu baba na baba wadogo leo wapo njiani wanakuja kulipa kisasi kwa jamii
yako yote, na ukiwashinda mababa ujue tu watoto na wajukuu wameshaanza
kufundishwa namna ya kutumia siraha watakuja kesho kulipa kisasi.
Hivyo
wao hupigana vizazi kwa vizazi na wakikushinda wakakuondoa kabisa baada ya muda
wanaanza kugeukiana na kupigana wao kwa wao wenyewe kwa visa vyao vya zamani
kabla wewe hujafika hapo.
MUHIMU
Fahamu kisasi ni kitamu nafsini mwa binadamu lakini kinamaliza mtu
taratibu sana hiyo inakufunza leo unapoingalia jamii ya taifa la waafghanistani
na nyingi baadhi ya hapa nyumbani Tanzania.
Kwa karne na karne nyingi kisasi hakimpi mtu suluhisho la kudumu au kumpa
tulizo nafsini la kudumu ila ukoleza moto na moto na kisha maangamizi kwako na
jamii zenu na mnayekosana naye.
MBINU
UNAWEZA KUTUMIA KUACHILIA/KUWASAMEHE WANAOKUUDHI (ILI KUONDOA KINYONGO/KISASI).
(..Kusamehe ni uamuzi wa kumwachilia
huru mfungwa, ambaye unagundua mfungwa huyo ni wewe mwenyewe." Lewis B. Smedes)
1 Kusamehe
kwa kuupuza (win-win)
Hii mbinu ya kupuuzia tunaitumia sana pasipo kujua
tunaitumia unakuta unatembea labda mtaani au hupo kwenye usafiri wa umma halafu
mtu anakukwaza kwa namna yoyote ikiwa kukukanyaga halafu anajifanya hana habari
anapita. Basi unachofanya unamuangalia tu halafu unacheka kidogo huku unatikisa
kichwa, halafu unaendelea na simu yako au kuongea na jirani yako.
Mbinu hii inasaidia pia katika mazingira na
mazingira tu hasa unapomuangalia mtendaji halafu unakataa kusababisha makubwa
kwa vitu vidogo vidogo, hivyo unapata ahueni flani yaani mimi mshindi hata kama
yeye kajifanya mshindi, siwezi poteza muda wangu kugombana na mtu asiyejielewa.
Wakati mwingine unaamua kuondoka na kwenda mbali kidogo na huyo anayekuudhi kwa
wakati huo.
Athari
ya mbinu hii pia
Inahitaji hekima sana namna ya kutumia mbinu hii na
pia inategemea na mahusiano na mtendaji na mtendwaji kutoa matokeo ya mbinu hii
Mfanyakazi na Bosi wake, Mume na mke na Mtoto na Mzazi. Si rahisi kumfanyia
bosi wako hivyo wakati anakuwakia kisawasawa au mume na mke sababu utakapotumia
mbinu hii ni sawa unamwaga petrol kwenye moto uwe na uhakika tu kutatokea
mlipuko zaidi.
2.
Kusamehe
kwa kulinda afya ya akili yako
Nakumbuka tulikuwa na mazungumzo na rafiki zangu niliokuwa
nasoma nao chuoni. Katika kujadiliana hili na lile, kuna mmoja wetu akatangaza
msamaha kwa kiongozi mmoja mkubwa nchini kwa sababu alizoziona yeye binafsi
zimemuumiza. Sasa mmoja akamuuliza vipi mkubwa! Kwani? hata ukimsamehe yeye ana
habari na wewe au anakufahamu. na yeye akamjibu ‘kwani kutoa msamaha anapata
faida nani? Ni mimi mwenye kubeba uchungu au yeye anayeendelea maisha yake
pasipo kuwa na tatizo lolote’.
Mbinu hii inasaidia sana kama unakuwa una uelewa
kukaa na kinyongo kwa muda mrefu kunakufanya uanze kuharibu afya yako mwenyewe
kwa magonjwa kama vile msongo wa mawazo (depression), kichwa na shingo kuumwa, tatizo
la mifupa, vidonda vya tumbo na macho kuanza sumbua kuona vizuri.
Msomaji wangu hapa sasa utapita mwenyewe gharama ya
kinyongo na ya kuachilia hipi unaweza ilipia?. Tafiti zilizofanyika hivi
karibuni zinasema asilimia 60 ya aina za kansa zinasababishwa na mtu kuwa na uchungu.
Kusamehe kwa matumaini.
(Kusamehe kwa kutumaini kunahitaji kubeba hekima na kutumia akili pia).
Ni rahisi sana kusamehe wale tunaowapenda na kuwajari sababu ya mahusiano yetu na wao. Tunasamehe kwa haraka sababu ya tumaini pengine hao wenza wetu siku za usoni watabadilika. Safari hii huwa ndefu kutokana na kuamini mtendaji siku moja atabadilisha mtazamo hasi au kile usichokipenda siku za mbeleni.
Uvumilivu, upendo na saburi ni moja ya vile vinavyotusaidia katika safari hii kupangua kila hoja ya machukizo na yale yanayotujeruhi kutoka kwa wale tunaowapenda kwakuwa hatutaki kuona wakiharibikiwa sababu upendo una nguvu sana kushinda mauti.
Ni safari ya matumaini inayohitaji sana hekima sababu wapo ambao wameweza kwenda nayo mpaka kupata matokeo ya kile walichokiamini lakini wapo walioishia njiani katika safari hiyo kwa kutumia hekima kuhusu kesho itakuwa vipi, na pia lipo kundi ambalo lilijitoa hadi mwisho na mambo hayakuwa sawa tena walijikuta na wao wamebeba mizigo ya wenza wao na pengine hivi sasa wanajutia kwanini wasingeishia njiani wakafanya mengine tu.
Kifupi kusamehe kwa matumaini kuna matokeo ya aina mbili hapo baadae yale tulioyatarajia na yale hatutayatarajia. Kama umebeba uvumilivu, saburi na upendo katika safari hiyo usiache pia hekima na akili nyuma.
4.
Kusamehe kwa imani.
“..Dini kubwa ulimwenguni zina mapokeo yanayobeba ujumbe wa msingi kuhusu Upendo, huruma na msamaha. vitu muhimu kuwa sehemu ya maisha yetu kila siku..” Dalai Lama
Kila imani ilumwenguni ina jambo la kueleza kuhusu msamaha na kuachilia pasipo kinyongo ili uweze kupokea thawabu kwa Mungu muumba mbingu na nchi. mfano
Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana
Hivyo unapokuza katika sababu moja wapo ya kusamehe waliokukosea unaweza kufanya hivyo ka kuangazia hasa maandiko ya imani na ukapata stamina ya kusamehe bure bila kutazamia chochote kwa binadamu mwenzako, ili uweze kupokea thawabu kwa Mungu.
Na kwa kutumia sababu au kigezo hiki kunaifanya ulimwengu wako wa ndani kusonga mbele.
5.
Kusamehe kutokana na upana wa uelewa wako juu ya maisha. (Hekima)
(“..Mimi siyo mtakatifu, labda ufikirie ni mtakatifu mwenye dhambi anayejaribu tu...” Nelson Madiba Mandela )
Napenda kuanza kwa kumnukuu waziri mkuu wa kwanza wa India bwana Mohandas Gandhi ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Mahatma Gandhi aliwahi kunukuliwa akisema
“..The weak can never forgive. Forgiveness is the attribute of the strong…” Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba watu dhaifu kamwe hawawezi kusamehe, kusamehe ni kwaajili ya watu wenye nguvu. Na nguvu aliyoizungumzia bwana Mahatma Gandhi ni ile hekima ya mtu kwenye fikra zake. Nianze kwa kutafsiri msamiati “hekima” maana yake
Tafsiri ya msamiati Hekima
Ni akili inayomwezesha mtu kufikiri na kuweza kutoa uamuzi unaofaa.busara au maarifa ya kufikiri na kuamua jambo linalofaa ambayo mtu huyapata kutokana na uzoefu wa muda mrefu. (Kamusi ya Kiswahili ya karne ya 21)
Kusamehe mtu na kutoa kinyongo ndani yako sio udhaifu ila inataka sana upana na uelewa wa fikra zako katika maisha. Pale unapoelewa madhaifu yako kama mwanadamu na kukubali kila mwanadamu ana mapungufu yake na kuhitimisha hakuna mkamilifu chini ya jua.
Pia unapofikiri kusamehe hakuwezi kubadili yaliyopita lakini kunatoa ongezeko katika kutazamia kesho yako kiafya, kifikra na kimaendeleo.
*Mwisho*
Maoni
Chapisha Maoni