Waelewe Wanaume (Understand Men)
Habari za muda kidogo
wasomaji wa makala ninazoziandika hasa kuhusu saikolojia na maisha karibu
katika makala inayohusu kuwaelewa wanaume.
Malengo ya makala hii
nimejikita katika dhana ya msingi ya kumuelewa mwanaume na hili itasadia katika
kuongeza hekima kati yetu sisi wanaume wenyewe kwa wenyewe katika kujielewa na
pia wanawake kupata mwanga kuhusu mwanaume kihasili hasa tabia na mwenendo wao.
Kuwa mwanasaikolojia
kunakupa ufahamu wa aina nne juu ya tabia za mwanadamu ikiwepo (i) kuelewa tabia, (ii) kuielezea tabia (iii)
kuitabiri tabia na (iv) kuidhibiti au kuiendesha tabia (control). Hivyo kuna
mambo mengi siwezi kufunguka kwa sababu maalum sababu ntakuwa nabomoa badala ya
kujenga hivyo kuwa na tahadhari kwangu ni muhimu sana kuliko mambo mengine.
Hivyo kadili utakavyokuwa
unatafakari unaposoma na kuingia ndani katika haya niliyoyandika ndipo utazidi
kufahamu tabia nyingi na kwa upana kuhusu Mwanaume katika maisha ya ndoa,
mahusiano, kiuchumi na pia jamii na tamaduni.
hivyo pia kupata busara
na akili ya kuishi na mwanaume katika familia na mahusiano pasipo mifarakano au
mikwaruzano ya mara kwa mara kupitia elimu hii na kuwaelewa pindi unapochukua
tahadhari nao.
TAFSIRI
MWANAUME.
Mwanaume ni
mtu aliye na jinsia ya kiume. (Kamusi ya kiswahili karne ya 21) pia Mwanaume au
mvulana mwenye aina tabia sifa kama vile uwezo na ujasiri au ushupavu.
ASILI
YA MWANAUME
i.
Wanadini
imani zenye mzizi ya Abrahamu (Ukristo, Uyahudi na Uislamu).
Katika imani zenye
mizizi ya abrahamu yaani ukristo uyahudi na uislamu inaeleza mwanaume au
chimbuko la mtu mwanaume linatokana na uumbaji wa Mungu na mwanaume wakwanza
alikuwa Adam alipewa kutawala viumbe vingine, kutunza
bustani na msaidizi wake ni mwanamke Eva.
Katika nadharia hii
kuna vitu vitatu vinajitokeza hasa kuhusu mwanaume
a)
Asili ya mwanaume ni kutawala
(dominate).
b)
Mwanaume ni kiongozi (leader).
c)
Mfanyaji kazi kiasili.
(worker)
ii.
Wanamapinduzi/wanaubadilikaji
(Wanasayansi na wasioamini katika Mungu)
Dhana hii ya wana
mapinduzi katika kutafsiri mwanaume ilihasisiwa na mwanabaiolojia Charles Darwin mnamo karne ya 19 hii kikmueleza
mwanaume asili yake ni kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyochukua miaka
mingi hivyo mwanadamu mwanaume ni mnyama au kiumbe jamii
Unaposema au kueleza
dhana hii katika muktadha wa msamiati Jamii ni lazima kila jamii kiasili ina
mpangilio Fulani kuitambulisha hasa za wanadamu ikiwemo uongozi na mfumo wa sheria
flani zenye kubeba utambulisho wa jamii hizo.
Kutokana
na dhana ya unyama unapata vitu vinavyojitokeza
a)
Mwenye nguvu mpishe.
b)
Kupambana kwa ajili ya rasiliamali
wakati wote ( resource).
c)
Samaki mkubwa ni halali kumla mdogo ili
aendelee kuwepo.
iii.
Tafsiri ya jumla inayopatikana.
Hivyo tunapoangalia
katika utangulizi hasa katika kufahamu tafsiri na asili ya mwanaume kutokana na
vyanzo vya imani pamoja na wanasayansi utagundua zipo sifa ambazo ni za kiasili
na pia kibaiolojia na kisaikolojia ambapo nadharia zote hizi mbili za dini na
wanasayansi au wanaubadilikaji wanazitaja.
Kila mwanaume anazo ila
katika kujidhihirisha kwake kwa kila mwanaume ni tofauti kutokana na nidhamu
ambazo kila mwanaume anazipata kupitia tamaduni imani malezi pamoja na
mazingira anayokulia au kuwepo.
iv.
Tofauti
ya mwanaume (manhood) na uanaume (masculinity).
Mtakubalina na mimi
katika haya machache hasa napotumia msamiati “kuwa mwanaume” kigezo
cha kitamaduni katika mtazamo wa jamii mbalimbali. Leo hii kuna msemo unaibuka
hapa nyumbani Tanzania kwenye uhususani kwenye mitandao kuhusu “mwanaume wa
dar” na “wa mikoani” huku wakijaribu kutofautisha kwa namna tofautitofauti.
Mtazamo wa uanaume ni
tofauti katika jamii mbalimbali mfano kuna jamii nyingine sifa mojawapo ya
uanaume inajumuishwa na suala la kutahiriwa na nyingine kutotahiriwa, zipo zinazosema
uanaume kuwa na wake wengi na nyingine kuwa na mke mmoja, pia zipo zinazovuka
mipaka hata kusema kulia sio uanaume.
Hivyo ni vigezo tu
lakini ni vya kitamaduni zaidi na lengo la makala hii ni kuangazia zile za
kiasili yaani mwanadamu wanaume anapozaliwa anakuwa nazo ila nidhamu
anayojifunza ndio inamsaidia kumtofautisha kimaamuzi katika kujidhihirisha kwa
tabia hizi.
FAHAMU
TABIA NA UASILI NDANI YA MWANAUME.
Hizi tabia haijarishi taifa kabila jamii tamaduni ila
kinachotofautisha ujihidhihirishaji ni ni nidhamu ya ujidhibiti au kujizuia
“self control” kunakotokana na malezi, tamaduni, mazingira na imani.
1. Kutungwa kwa mimba.
Tulifundishwa katika
ngazi mbalimbali za kielimu kuhusu Kromosomu tafsiri rahisi hili azaliwe mtoto
mwanaume ina maana baba anapotoa mbegu ya kiume yenye kromosomu X ina maana
mtoto anakuwa wa kiume sababu mama (mwanamke) yeye huwa na kromosomu Y tu ila
mwanaume yeye anazo zote mbili yaani ile kromosomu X na Y hivyo kuzaliwa mtoto
wa kike au wa kiume hutegemea baba anatoa kromosomu gani.
(Unapata jibu mwenye
kusababisha mtoto azaliwe wakike au wa kiume ni baba (mwanaume)
Hivyo kromosomu XY
(Mwanaume) inaelezwa na wanasayansi kuwa na mapungufu kutokana na X hivyo si sawa na hile yenye YY (Mwanamke).
(Picha inayoonesha shughuli watoto wa kiume wanajishughulisha wakiwa
katika umri)
Hivyo mapungufu hayo
yanafanya pia idadi ya wanaume kuwa wachache kuliko wanawake. wanaoweza
kuhimili kuishi “survive” wakiwa watoto na kukua ni wakike kuliko wakiume kwa
mujibu wa tafiti.
Ijapokuwa watoto
wanazaliwa wengi wakiume kuliko wakike. lakini shughuli, michezo ya hatari na
majukumu hasa kwa watoto wakiume katika jamii mbalimbali inasababisha watoto
wakiume kuwa katika hatari nyingi na mazingira hayo, na hivyo idadi yao kuwa
chache sana ukilinganisha na wale wa kike.
(Picha inayoonesha shughuli ambazo watoto wakike wanajishughurisha
muda mwingi wakiwa na umri mdogo mmoja kambeba mdogo wake na wapo karibu na
jiko nyuma yao)
Changamoto hii mara
nyingi hujidhihirisha wakati wa kipindi cha kuoa na kuolewa sababu watoto
wakike pia wanapofikia kipindi hiki mapema tofauti na wa kiume na hapo uchache
ndipo unajidhihirisha.
2. Akili ya mwanaume na uongeaji.
“Kuna msemo mmoja
unasema wanawake zaidi ya watatu wanapokuwa katika mazungumzo ni umbea lakini
wanaume zaidi ya watatu wanapokuwa katika mazungumzo wao wanapashana habari”
(Tafiti zinabainisha kwa siku mwanaume huongea maneno 7000 na
mwanamke uongea maneno 20,000)
Katika kipengele hiki
tunajifunza kifiziolojia utendaji wa ubongo wa mwanaume unaegemea sana katika
upande wa kushoto na wanawake kwao ni upande wa kulia.
Utendaji wa akili hasa
katika upande wa kushoto tunauita wenye kuwezesha fikra na mawazo mantiki
“logic” na wenye uchanganuzi sana wa mambo.
lakini ule wa
upande wa kulia wenyewe uwezo katika fikra au mawazo ya ubunifu, uelewa wa
masuala kiasili (shuku)
Kwahiyo kwa dhana hii utajifunza kuwa mwanamke huwa muongeaji sana
kuliko mwanaume hilo ni suala la kimaumbile.
Pia mwanamke anauelewa
mkubwa sana wa kiasili “intuitive thinking” kushinda mwanaume na ndio sababu
mtoto wa kike kumtuma akakuelewa akiwa mtoto wa miaka mitatu ni mkubwa kuliko
kwa mtoto wa kiume.
Mtoto wa kike hata
unaweza muachia mtoto mdogo akakaa nae akamuangalia bila shida yoyote.
Pia uwezo wa kuanza
kuongea kwa mtoto wa kike anaanza mapema kuliko wa kiume.
Pia unajifunza suala
jingine hasa katika mahusiano mwanamke anafikia ukomavu wa kifikra na mawazo
akiwa na miaka 22 na anaweza kuolewa na akatunza familia vizuri wakati kwa
mwanaume ni kuanzia umri wa miaka 27 ndio anafikia kiwango hicho cha kukua kifikra.
Mwanamke na mwanaume
wanapolingana kiumri kiasili mwanaume ni mdogo kwa mwanamke.
Unajua sasa
kwanini mwanaume anachoshwa haraka na mwanamke anaeongea sana?
3. Ukali (Aggressiveness).
(Wavulana wakipigana, tazama wanaowagombelezea wakike anamaanisha
kuwaachanisha lakini wakiume anafanya kwaajili ya picha wengine wakiume
wanashuhudia pambano)
Tafsiri ya neno
aggressive inapokuja katika lugha ya Kiswahili haileti ladha kamili hasa katika
upande wa saikolojia ijapukuwa inatoa muelekeo wa kidhana
Aggressive ni “ushari”, “gomvi”, “chokozi” “jeuri” na tafsiri nyingine
ni “kutaka maendeleo”.
Hivyo kila mwanaume ana hali hii kiasili himo ndani yake ila kujitokeza
kwake kunatokana na nidhamu katika imani tamaduni au mazingira huo unakuwa ndio
msingi wa kujidhibiti au kujiachilia.
Kwanini basi hali hii hipo kwa wanaume? Sababu ya homoni inayoitwa
Testosterone homoni hii huwa katika viungo vya uzazi wa mwanaume na ndio
inayomtofautisha mwanaume kitabia na mwanamke.
(Donald Trump anaelezwa kuwa ni moja ya watu wenye
viwango vingi vya testosterone katika mwili wake)
Je nini kinachotokea homoni hii inapozidi? Tafiti zinabainisha kuwa
wengi wenye homoni hii iliyozidi huwa na hali ya kupambana sana kimaisha homoni
hii inafanyika kama kumpa motisha ndani yake. Ndio maana matajiri au mabosi
wengi huwa ni wakali na pia wengi ni wanyanyasaji wa kijinsia “womanizer” sababu
tafiti wengi huwa wana homoni hii iliyozidi.
Lakini changamoto hasa watu wengi sana wanaozidiwa na homoni hii hasa maeneo
ya afrika na asia huishia kuwa na wanawake wengi.
Na pia kuwepo kwa homoni hii kunasababisha pia matukio mengi ya uharifu
kwa mujibu wa takwimu, matukio ya uharifu utekelezwa kwa asilimia kubwa na
wanaume kuliko wanawake.
(Swali kwa wasomaji wanaume na wanawake? Je sinema
gani kati ungepata shahuku ya kuanza itazama )
Pia kujidhihirisha kwa homoni hii inafanya wanaume wengi sana kupenda
michezo au filamu zenye mapigano mfano Vita, ubabe, na michezo kama ngumi. Na
hata kuwa washabiki sana pale mazingira ya ugomvi unapotokea kuliko kusuluhisha
au kuamulia.
4. Utawala (Dominance)
(Picha askari wa uingereza wakielekea vitani
pembeni ni wake zao (mtoto akimkimbilia baba yake). Kwa karne nyingi matukio ya
vita yalihamasishwa kwa kauli mbiu ya wanaume kupigania uhuru wao, wake na
vizazi vyao dhidi ya maadui wa nje.)
Tafsiri yake ni kitendo cha kuwa na amri juu ya au amuru au mamlaka.
Kama nilivyojaribu kupitia nadharia mbili ya asili ya mwanadamu hasa mwanaume
zote kwa pamoja zinabainisha kuwa kila mwanaume anakitu kutawala ndani yake
haijalishi umri wake.
Kupitia nadharia hii
mwanaume kiasili anawajibika kwa ajili ya jamii yake katika kuilinda na
kuipigania dhidi ya matukio mbalimbali katika ulimwengu mfano uharifu, majanga
na vita
mfano Baba ujiona
anawajibika kwa ajili ya familia yake mkewe na watoto pia kila kijana wa kiume
hujiona ana wajibu kuwalinda dada zake. Hivyo suala hili ni la kiasili kabisa.
Hivyo katika hili
unapata kufahamu kwanini jamii nyingi zina tamaduni mfumo dume yaani zinazowapa
wanaume kipaumbele au mazingira pendelevu.
Utajifunza kosa kubwa
mwanamke analolifanya kwa mwanaume ni pale kumvunjia heshima au kutomuheshimu
mume wake au kaka yake au mtu yoyote kaitka jamii ambaye ni jinsia ya kiume.
Ukitaka kuutikisa moyo wa mwanaume kwa muda muoneshe kumheshimu (hii kwa wanawake).
Pia kwa sababu hii
utagundua kuna jambo linajichipuza nalo ni “Wivu” hivyo si jambo la kawaida
kukuta mwanamke ameolewa na wanaume watatu wakaishi pamoja lakini mwanaume kuoa
zaidi ya watatu ni jambo la kawaida kwa tamaduni nyingi duniani.
Pia utafahamu wanaume
kwanini huwa hawaaminiani wao kwa wao kuhusu mwanamke.
Wivu ni kitu kipo pia
kwa kila mwanaume.
5. Mwanaume huvutiwa kwa kutazama.
(Picha ya mchoro inayomuonesha mfalme Daudi akimwangalia mwanamke
anayeoga (Mke wa kamanda wake “Uria Mhiti”) baadaye alimtwaa na kuwa mke wake
baada kutengeneza mazingira ya Uria Mhiti kuuliwa vitani Ghadhabu na adhabu ya
Mungu ikawaka juu ya nyumba ya Mfalme Daudi.)
Picha ya kielelezo hiki nimemtumia Mfalme Daudi kama kielelezo kuwa
mwanaume yoyote anaweza kukumbana na hali ya uzinzi au uasherati kama
akijisahau katika nidhamu ya kudhibiti macho yake.
Niliwahi kumsikia dada
mmoja ambaye alikuwa na ghadhabu sana kutokana na tabia ya mchumba wake, hasa
wanapotoka yaani ni rahisi sana kugeuka geuka wanapopita wadada wengine kwahiyo
alishindwa mvumilia kabisa kutokana na mara kwa mara kuongea nae laikini tabia
hiyo ilikuwa inajirudia baada ya muda hivyo aliafikia kuachana nae na kuvunja
uchumba.
Labda nirejee sehemu ya
utaangulizi nilipoeleza kuwa utofauti wa wanaume na asili yao hutokana na
nidhamu ambazo kila mwanaume anazipata anafundishwa anajifunza kupitia
tamaduni, imani na malezi pamoja na mazingira anayokulia au kuwepo.
Hivyo tamaa ya kuvutiwa
kwa mwanaume hasa kwa wa jinsia nyingine ina nguvu sana machoni, ila kila
mwanaume ana nidhamu ya kujidhibiti kwa namna tofautitofauti.
a)
Mwanaume ni rahisi kumpenda mtu kwa
uzuri au kwa kumuona tu lakini kwa mwanamke yeye anaegemea sana hisia zake na
mara nyingi hisia utegemea ukaribu wa kipindi Fulani au kwa kusikia tu habari
za mtu Fulani. Lakini mwanaume inamtokea tu kwa kuona sababu tamaa ya wanaume
hipo machoni.
b)
Vilevile utajifunza kwanini
wanawake wengi hupoteza mvuto kwa wanaume zao baada ya kuwaoa? Sababu wanawake
wengi hawafahamu mawanaume huvutiwa na muonekano (physical appearance) na
wanawake wakishaolewa huwa wanaacha kujari muonekano wao tena mbele za wanaume
zao.
c)
Pia kwa kigezo hiki unajifunza
kwanini wanaume hunaswa kirahisi na wanawake wanaovaa nguo za utata na kujiremba
lakini wake zao wanapoondoka baada ya mifarakano hupata tabu sana na kujaribu
kutafuta suruhu nao baada ya kutafakari sana kuhusu kutaka na kupenda kupi
muhimu.
Sababu moyo wa mwanaume
hutamani wengi lakini upendo wake huwa sehemu moja.
(Pia tunajifunza katika vitabu vya imani kupitia mtoto wa kwanza
Reubeni wa mzee Yakobo (Israel) alivyojikuta akiingia katika mahusiano ya
kimapenzi na mama yake Mdogo Bilha ambaye ni mke mdogo wa baba yake).
Hivyo ni muhimu sana
kwa kijana wa kiume kujifunza kuwa na nidhamu ya udhibiti wa macho yako itakujenga
katika nidhamu ya kuutawala mwili wako kihisia si kila kitu lazima utazame tu
kama hupo katika maisha ya kimalengo juu ya kesho yako (si vijana wengi wakiume
wanaishi kimalengo).
Kijana wa kiume kuna
mazingira mengine huwa yanatokea usijiamini kupita kiasi, sababu Duma na swala
hawawezi kuishi kwa karibu halafu lisitokee lakutokea.
6. Shawishi au shawishika (Persuade)
(Picha hii inaonesha tukio la kijamii linalohusu upimaji wa afya.
Angalia je waliojitokeza kuhudhuria idadi hipi ni kubwa? katika ya wanaume na
wanawake.)
Wengi tunaoudhuria
katika shughuli mbalimbali za kijamii mfano zili zinazohusisha labda uchangiaji
damu, upimaji wa afya, semina, misiba, mikutano ya kidini utagundua idadi kubwa
sana ya wahudhuriaji wakubwa au kwa idadi kubwa ni wanawake kuliko wanaume.
Kama ujawahi fanya
tafiti hiyo hanza kuanzia sasa kama ni kanisani (sababu jumuiya hii uwachangamanisha
watu wa jinsia zote mahali pamoja) tofauti na jumuiya za imani nyingine. utagundua
kundi la wanawake huwa ni kubwa sana. Basi umeshawahi jiuliza kwanini?
Kama nilivyoelezea pia
katika sababu mojawapo inayowatofautisha wanaume na wanawake kiakili wanaume
hutumia zaidi sehemu ya ubongo wa kushoto. Hivyo kumshawishi mwanaume katika
shughuli za kijamii kunahitaji sana sababu za kimantiki katika fikra zake na za
kujitosheleza au pengine kama kuna manufaa au kumuinulia shauku.
Hivyo muhimu cha
kufanya kama unaosoma ujumbe huu ni mwanamke umeolewa fanya hivyo vya msingi
kwanza baada ya yeye kuona manufaa, mantiki au kupatwa na shauku basi utamvuta
lakini kumbembeleza au kumlazimisha hakuwezi kuleta muafaka anaweza kufanya
kukufurahisha tu kwa muda huo lakini si kwa kudhamiria.
Hata katika saikolojia
ya matangazo sababu njia moja ya kujaribu kushawishi jinsia zote katika
biashara hutumia wanawake wazuri ili kupata uangalifu wa mwanaume katika kuuza
na kutangaza bidhaa zao.
Maoni
Chapisha Maoni