Jifunze mambo yatakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha duniani (Finland Nchi yenye watu wenye furaha duniani?)
Saikolojia:
Jifunze mambo yakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha duniani ( na fahamu vigezo
vilivyotumiwa kuichagua Finland kuwa nchi ya kwanza (Juu) kwa watu wenye furaha
na Tanzania ya tatu (kutoka mwisho).
“..Katika makala hii
nimejikita kuchambua vigezo vilivyoifanya finland kuwa nchi ya watu wenye
furaha kama Case study na kisha kuangazia sababu...”
1.
MWANZO
Wanavyoeleza
wanafalsafa na wasaikolojia kuhusu dhana ya kuwa na Furaha ni nini?
Dhana ya tafsiri kuhusu
nini maana ya furaha imejadiliwa sana Duniani kuanzia katika mataifa mbalimbali
ulimwenguni kwa watu wa dini, wanafalsafa na mwishoni mwa karne ya 20 ikachipukizia
kwa wanasaikolojia mfano William James (1842-1910) “Functionalism school of thought” na Abraham Maslow (1908-1970) wa “Humanistic School of thought”.
i.
Falsafa
Katika
Falsafa (Philosophy) tafsiri
ya msamiati furaha ni kuishi maisha mazuri au yenye ustawi mzuri ambapo kwa
wagiriki utumia msamiati “eudaimonia” ambapo wanasisitiza furaha
ni kuwa na maisha mazuri na maisha mazuri ni maisha yenye maadili mema.
Hivyo kwa maelezo
mafupi, Plato Socrates na Aristotle wanaweka hitimisho katika suala la kuwa na
maisha mazuri(Furaha) na yenye ustawi ni nini? Ni pale mtu, watu au jamii
inapotaafuta kuenenda au kuishi maisha ya maadili/maadili mema ndipo kuna
kustawi na kuwa na furaha kunapotokea ndani yao.
ii.
Saikolojia
Katika
Saikolojia (Postive Psychology)
Furaha tafsiri yake ni kuwa na hali njema na ustawi katika akili na kihisia
ambao wanaokuzunguka kukutafsiri mtu chanya au mwenye furaha.
iii.
Tafisri
nilizozipata
Kwa kujumuisha
falsafa, saikolojia na maandiko vitabu vya Mungu ili huwe na furaha ya kweli na
kudumu inaanzia na wewe kwanza kubadilisha mfumo wa maisha yako kabla ya
kumbadilisha mtu mwingine au mazingira yako ya nje.
iv.
Baadhi
ya Vigezo vilivyotumiwa katika kuchagua nchi yenye furaha duniani kwa mujibu wa
ripoti
a)
Upatikanaji wa msaada kwa mtu kutoka
katika jamii inayokuzunguka hasa wakati wa uhitaji.
b)
Kutokuwepo kwa vitendo vya rushwa
c)
Hali ya uhuru katika Jamii
d)
Matendo ya ukarimu na msaada kwa
wahitaji
2.
FINLAND
TAIFA LINALOONGOZA KWA KUWA NA FURAHA ULIMWENGUNI. (CASE STUDY)
i.
Ifahamu
Finland kwa ufupi ilipotokea karne ya 20.
Finland mwaka 1993
tafiti zinasema iikuwa taifa lenye visa vingi vya ulevi kupindukia na watu
kujiua na hali ya uchumi mbovu ulioharibika hii baada ya uhuru wake baada ya
kuvunjika kwa Soviet Union (USSR).
(Baadhi ya picha za matukio katika vita ya kati ya Finland na
Soviet Union “Winter War”)
Ikumbuke mwaka 1939
taifa la Finland lilikuwa katika vita na Soviet Union (USSR) katika kujitetea na sera ya utanuzi mipaka
(expansionism) wa Soviet katika magharibi mwa mipaka mwa nchini Finland.
Finland kwa kuwa
kiuchumi na kimabavu hisingeweza kuishinda ili kurudisha mipaka yake iliyoiochukuliwa.
Hivyo Finland ikajikuta inaingia katika mapatano na Nazi ujerumani chini ya Adolf
Hitler katika kushirikiana kivita (Mutual Alliance) katika vita dhidi ya Soviet
Union (USSR) ili kurudisha sehemu ya nchi yake.
Ili iweze rudisha
mipaka iliyoipoteza katika vita “winter war” bahati mbaya sana kwa
Finland vita ikawa kinyume cha Adolf
Hitler na washirika wake hivyo
kushindwa kwa Hitler ndio ikawa
anguko kamili la Finland yote na uhuru wake katika makucha ya Soviet
union (USSR). Hivyo hali zao zilikuwa si nzuri kama hilivyokuwa kwa mataifa
yote chini ya umoja wa nchi za kisovieti hadi kusambaratika kwa umoja huo
mwanzoni mwa miaka ya 1990.
ii.
Finland
hilipo sasa.
Mwaka huu 2018 taifa la
Finland ndio taifa ambalo limetangazwa kuwa na watu wenye furaha sana kimaisha
wakati huo Tanzania ikiwa chini sana ya tatu kutoka mwishoni katika viwango vya
mataifa ya watu wasiokuwa na furaha.
katika ulimwengu. Kwa kweli baada ya kusoma ripoti hiyo ilinifanya
kwanza na mimi niangalie ni vipi taifa hilo limefanikiwa kuwa nafuraha katika
ulimwengu. Kama Mwanasaikolojia na mpenzi wa kujifunza na pia kusoma falsafa za
maisha nikatamani nifahamu hivyo nikaanza kupekua pekua vitabu vyangu ili iwe
rahisi kupembua kwa mapana kuhusu dhana ya furaha na maisha mazuri huku
nikijifunza kupitia Finland.
iii.
Baadhi
ya sababu zilizoifanya Finland kuwa taifa la watu wenye furaha kwa mujibu wa
tafiti.
(kwa
tafiti zilizotolewa na IMF 2017 Finland haipo katika 30 bora ya nchi (1)Tajiri
wala (2) zenye uchumi mkubwa duniani. Ni nchi yenye wakazi wengi wa kipato cha
kati au wastani)
a) Viwango
vidogo vya rushwa katika serikali yao (Rushwa inapokuwa viwango vya chini Haki
inatawala).
b) Uwepo
wa bendi nyingi za muziki (Heavy Metal Bands)
c) Mfumo
bora wa elimu hasa kwa masomo ya sayansi kusoma na mathematics
d) Taifa
linaloongoza kwa kunywa kahawa ulimwenguni hivyo kipindi cha winter huwa
hawasumbuliwi na baridi
e) Ni
taifa lenye utulivu ikiwemo viwango vya chini vya uharifu, rushwa na hakuna
eneo ambalo haritawaliki au kushindwa fikiwa na serikali katika huduma muhimu za
kijamii.
f) Uwepo
wa tamaduni
ya Sauna kwa taifa lote (Sauna ni aina ya vyumba vya mvuke wa moto
viavyotumiwa kuliwadha wakati wa baridi).
g) Taifa
lenye viwango vya chini vya vifo vinavyotokana na uzazi na yanayohusu wamama
wajawazito hivyo ndio taifa zuri kwa mtu kuwa mama na kuwa na familia.
h) Ni
moja ya Taifa linaloongoza kwa unywaji wa maziwa ijapokuwa pia ni taifa la kumi
na moja duniani “kugida bia”.
i)
Mji wake mkuu Helsinki ni kati ya miji
mikuu inayoongoza na kuwa na watu waaminifu utafiti uliofanywa katika mitaa ya
miji hiyo kwa wakati tofauti tofauti ziliangushwa wallet 12 lakini 11
zilirudishwa kwa wenyewe na nyingine haikurudi.
j)
Ni moja ya taifa linaloongoza katika
uazimishaji na usomaji wa vitabu. Wastani wa vitabu 100 kwa kila mwaka kwa kila
familia ya nchi hiyo.
“Furaha
inaanzia ndani ya fikra kabla ya kuathiriwa hasi au chanya na mazingira
unayokabiliana nayo
Je unajua?
nchi zenye vita Libya (70/156) na Iraq (117/156) zimeipiku Tanzania (153/156)
kwa kuwa na watu wenye furaha duniani. “
3.
BAADHI YA MAKOSA TUNAYOYAFANYA
KATIKA KUTAFUTA FURAHA
i.
Mtu
mwingine kukupa furaha.
(Mahusiano yoyote (Urafiki,Ndugu,
familia na kazini) ni kama akaunti ya
uwekezaji usitarajie kupata furaha kwa mtu kama wewe haujawekeza hisa ya furaha
katika akaunti ya mahusiano “reciplocity”)
Sehemu
tunayofanya makosa katika jamii zetu watanzania wengi sana ni kuamini katika
watu wengine kuwa sababu ya furaha kwetu
Wengi
wwaliovunjika moyo na kukata tamaa katika mahusiano walitarajia ndoa kuwa
sababu ya kufurahi kwao
Mfano
Viongozi, Ndoa na Marafiki nk ukweli ni kwamba furaha ni kitu ndani ya nafsi
yako kama unategemea sana watu wakupe furaha katika maisha yako. Pasipo wewe
mwenyewe kuwa sababu ya furaha hiyo ni kama unapoteza wakati wako au tarajia
kuvunjika moyo au matarajio yako “Disappointed” pia fahamu na ujifunze
kumuwekea tumaini kiongozi yoyote au mwanadamu mwenzako sana hupo njiani kuishi
bila furaha na kukosa utulivu ndani yako.
Formula ni hivi hisia chanya au
hasi zinatabia kuambukiza au kuambukizwa kustawi au kusinyaa kutokana na watu unaochangamana
nao “interacting”
“..Msimwekee
kiongozi tumaini...” <Mika7:5>
ii.
Kutarajia
Vitu (material things) vitakupa furaha.
(Nchini China mwaka 2012 kijana wa
miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Wang haliuza figo ili apate fedha kununulia
i phone na i pad)
Jifunze
kitu kwa mara ya kwanza ulipopata simu, gari, nyumba au kitu chochote cha ndoto
yako hali uliyokuwa nayo (mimi binafsi siku ya kwanza nilikosa usingizi kabisa)
halafu tafakari leo hapo hulipo. Jiulize kiwango cha furaha yako kipo sawa sawa
na siku za hapo mwanzoni hulipokipata? au siku ulipompata huyo Mr/Mrs right
wako? .
Ukishapata jibu sahihi basi fahamu wanadamu
tunakitu ku “cope” na hali. hii ndio inatufanya kila leo kuwa katika safari
ndefu ya kutafuta furaha katika vitu (Material things) na kamwe tunakuwa
hatuliziki na wenye mashindano sana yasiyo na tija yoyote na mara nyingi
yametuacha kuwa na majuto ya muda mrefu sana au kushindwa tafsiri furaha hipo
katika vitu hitaji? au tumizi?.
iii.
Kutafuta kukubalika
au kupendwa na kila mtu.
(Msichana Sahar Tabar(Kulia) alifanya Cosmetic Plastic surgery
ili awe na muonekano wa Angelina Jolie pengine ndiyo furaha yake ilipokuwa?
Furaha yako hipo wapi?)
Kwa mujibu wa tafiti
sehemu mojawapo inawafanya watu kutokuwa na furaha ni kutokana kutokubaliana na
mwonekano wao kisura na kimaumbile hadi jinsia (Transgender na transsexual) zao
hivyo imewafanya wengi kujaribu kujibadili ili kuboresha namna ya muonekano wao
hata kwa kutumia vipodozi vyenye kemikali zenye nguvu.
lakini pia tafiti zinasema wengi huishia katika
kujiua wanapogundua wameharibu zaidi au wamepotea katika hayo mengi
waliyofikiria hapo awali kabla ya kufanyiwa operation au kubadili jinsia zao.
Sababu moja iliyo kuu
ni kujaribu au kutafuta kukubalika, kupendwa na kila mtu au kutaka sifa kutoka
katika kila mtu kwenye jamii yako ni mtego sana. Kifupi huwezi kupendwa na kila
mtu katika jamii yako inayokuzunguka hata kama ungefanya vipi lakini kulinda
afya ya akili yako tafuta kufanya mema na yenye maadili na maamuzi mazuri ili
kusudi kama wapo watu wakina “melancholic” wasipate sababu ya
kukuchafua ili wapate wakuwasapoti katika chuki zao juu yako
Furaha ni sababu
zinazotokana na ndani ya mtu kwanza kabla ya za nje kufanya kazi.
iv.
Matumizi ya
vilevi na madawa ya kulevya kukupa furaha.
(Vijana wengi huingia katika matumizi
ya madawa ya kulevya katika kutafuta furaha na kujiliwaza).
Ningeanza kuelezea “alosto” au “kupata
stimu” ni kitu gani kisayansi
Ni pale vilevi au madawa ya kulevya
(psychoactive drug) katika utendaji kazi wake kwenye ubongo kwa kuzuia
utumikaji kwa kemikali Neurotransmitter ambazo zinaitwa dopamine,
norepinephrine na serotonin katika mfumo wa neva katika mwili.
(kutolingana “imbalance” kemikali
“dopamine, norepinephrine na serotonin” nisababu ya magonjwa ya akili mengi
baadhi yanahusiana na mood ya mtu mfano Bipolar disorder)
(Ugonjwa wa akili Bipolar Disorder unatajwa kuwa sababu ya tabia
za Chris Brown ikiwemo kupigana na kupiga watu Baba yake wakambo ni moja
waliowahi kupigwa naye )
Hivyo zuio hilo la matumizi ya kemikali
hizo zinafanya kuwepo kwa wingi wa neurotransmitter hizo katika Ubongo hivyo
kuathiri mfumo mzima wa utendaji wa kazi (sympathetic division, autonomic nervous
system).
Madhara yanatokea ikiwemo uongezekaji wa
mapigo ya moyo na upumuaji mboni kuwa pana na kuongezeka sukari katika damu
ikiambatana kukosa appetite.
Hivyo utumizi huo baada ya muda
unasababisha hali tegemezi kisaikolojia (Psychological) na kimaumbile
(Physiological) na kusababisha madhara katika akili na utendaji wa mwili
kikawaida hasa alosto inapoondoka muda baada ya kujidunga au kutumia kilevi au
madawa hayo.
Kifupi kutafuta kuliwazika, furaha au
burudiko la namna yoyote kwa njia ya vilevi na madawa ya kulevya ni sawa kutaka
maliza kiu cha maji kwa kunywa maji ya bahari inakuwa kwa kadili unavyoongeza
kasi uikate kiu ndio unavyokaribia mauti yako.
v.
Umaarufu
na kuwa na pesa nyingi.
(Kelvin Cubain muigizaji wa filamu za “Home
Alone” licha ya kuupata umaarufu ulimwenguni kote na kuwa na pesa nyingi akiwa
na umri mdogo, kwa sasa ameangukia na matatizo ya utumiaji wa madawa ya
kulevya)
Katika masuala ambayo
wanasaikolojia (Marekani na Ulaya) wanaendelea kuyafanyia utafiti ni pale
kwanini watu wengi ambao ni maarufu wenye fedha nyingi na ambao tunadhania
wanaishi maisha yenye kila kitu (Perfect life) katika jamii zao kuamua kujiua.
licha ya kuwa na vitu vingi vya anasa vinavyotamaniwa na kila mtu na fedha
nyingi wapo wanaoishia kujiua au kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya
au kuugua magonjwa ya akili hasa Msongo “depression”.
Hata hapa nyumbani
wengi tumeshuhudia katika kesi mbalimbali za watu maarufu wakiwa na mashtaka ya
matumizi ya madawa ya kulevya.
Katika jarida moja nchini marekani inabainisha kuwa nchi
zenye watu wenye kipato cha juu au hadhi flani na sababu kubwa inasemekana
wengi wanashindwa kukubaliana na hali zinapobadilika au kushindwa kwa kushuka
chini.
Hivyo fahamu umaarufu na pesa (Ukweli tunahitaji pesa sababu
ni ulinzi kwetu) lakini kupata vyote hivyo sio sababu ya kuwa na furaha kamili
na kujitosheleza katika maisha ni zaidi ya hivyo.
vi.
Kuwa
matarajio au kunuia matarajio au ndoto kubwa kuliko uhalisia.
(Rudolf Hess baada ya matarajio yake kushindwa akiwa bado mtu wa
pili katika Chama cha Nazi chini ya Adolf Hitler tu, mwaka 1941alifanya misheni
ya hatari kuruka na ndege binafsi kwenda Uingereza (wakati nchi zikiwa kwenye
vita ya pili ya dunia) kwa lengo kutafuta amani na suluhu na Uingereza
(Ijapokuwa Hitler baadaye alikaliliwa kuwa hakumtuma na aliagiza auliwe popote
atakapopatikana ). Baadae alipatwa na ugonjwa wa akili “paranoia”)
Kweli kuwa na ndoto
kubwa katika maisha ni jambo zuri sana na tena ni msingi mzuri katika kutupa
matumaini mbalimbali kuhusu kesho yetu. Sababu tumaini ni kuwa kuota ndoto
pasipo kuwa usingizini. Hili kutimiza ndoto zetu ni si tumaini tu linahitajika
bali Upendo na Imani. Upendo Imani na tumaini kwa pamoja
vinapofanya kazi ndani yetu vinatusaidia sana kuwa katika matarajio yenye
uhalisia.
Kuna kitabu kimoja
niliwahi kukisoma kulikuwa na utafiti uliofanya na chuo kikuu cha Havard
nchini marekani katika utafiti huo wanaeleza mara nyingi uchaguzi wetu katika
masuala tunayotazamia kutupa furaha katika maisha asilimia kubwa wengi
huafanya uchaguzi sio sahihi (kukosea.)
Hivyo sio kwamba hata
mimi hayajanikuta hivyo kisehemu hiki nina kiuzoefu. Kwahiyo wakati wote jaribu
kupembua matarajio yako kusudi yawe na uhalisia na kipawa uwezo ambao Mwenyezi
Mungu amekupatia. Kusudi husije ukapita katika kama hii huwa inasumbua sana.
Hali hizi huwakuta wafanyabiashara katika wakati wa kupanga maamuzi, Wanafunzi
katika kusubiria Matokeo yawe kidato cha nne au sita, hata wachumba wanapokuwa
wanafikiria maisha ya ndoa hapo baadaye.
Maoni
Chapisha Maoni