Mbinu za Kukusaidia kuishi kwa Furaha maishani
SABABU
ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUKUJENGA NA KUYAFURAHIA MAISHA.
Katika sehemu ya kwanza niliangazia sana “baadhi
tu” ya maeneo ambayo tunakuwa tunayatarajia sana kama ndio sababu kuu
sana kuja kutupa maisha mazuri na yenye furaha. Na nikitoa mifano halisi na
tafiti mbalimbali ambazo zimewahi kufanyika ulimwenguni kote hasa kuhusu
vipengele au vipaumbele ambavyo tumeviweka maishani kwetu kama sababu ya
kutufanya tuwe na furaha lakini sio.
(Hakuna kitu nimefundisha
na kukiandika kama hakina ushahidi wa kitafiti kutoka kwa wanasaikolojia na
wanasayansi)
Basi katika sehemu hii ya pili pia nimeangazia tabia
au matendo na mwenendo ambao unaweza kukusaidia kuwa na maisha yenye furaha
kama ukusoma sehemu ya kwanza jitahidi upitie ili hiwe na rahisi kwenda pamoja nikirejea
ripoti ya taifa la Finland mshindi wa mwaka 2018 kama taifa la watu wenye
furaha duniani.
Pia ili huweze kufuatilia vizuri
mafundisho haya kuhusu Saikolojia na maisha ni vizuri kama utaanza ni follow
katika akaunti yangu “Education mentor”.
Na pia kuhusu Maswali yoyote ya kisaikolojia na maisha unaweza
niuliza PM na mimi ntayajibu kwa mfumo wa makala au “mada” kipengele natazamia sana kukianzisha siku za usoni.
Basi tuendelee katika
sehemu ya pili ya kuhusu mada ya “Furaha”
(Kuwa na furaha ni uchaguzi wa mtu katika maisha)
1.
TABIA
YA KUWA NASHUKRANI NA KURIDHIKA. (GRATITUDE AND THANKFULNESS)
(“Kama
ukiwa unazingatia katika kutafuta mema na mazuri katika hali zote, basi
utagundua maisha yako yanajazwa na moyo wa kuridhika na kushukuru, hisia ambazo
zinaistawisha roho yako” Rabbi Kushner)
Hakuna anayependa umasikini
(hata mimi sipendi) au hali yoyote kinyume na mtazamo wa jamii kuanzia
darasani, kazini na hata katika muonekano wetu mbele ya jamii. Kila mtu
anapambana katika maisha kuwa katika hali bora kila leo lakini tunapopambana
kuna umuhimu tusiache nyuma “uhalisia”
au “uhalisi wetu” kama nilivyoeleza katika sehemu ya kwanza ya makala.
Bado mpaka leo huwa
namkumbuka sana binamu yangu katika safari yake ya kutafuta furaha hilipoishia
vibaya pasipo matarajio ya familia na wengi tu wakati huo mimi nikiwa bado
mdogo sana sijafika hata darasa la 6. Kwa kifupi nina binamu yangu alikuwa
kweli kajaliwa “kuwa na akili sana darasani” lakini kuna mtu mmoja ambaye
alikuwa anamsumbua sana anashindwa mpita tu yaani yeye alikuwa anakesha na kusoma
sana ili hawe mtu wa kwanza lakini hakuwahi kufua dafu ripoti zote za mihula.
Lakini miaka yote hadi
kidato cha tatu hakuwahi mpita. Basi kwa kuwa target ya furaha yake aishike
nafasi ya kwanza hata mara moja tu. Hivyo akapata watu waliomshawishi akisoma
achanganye na bangi kidogo ukweli baada ya hapo akawa mlevi kamili “addicted”
tangia hapo hakuweza fikia ndoto zake nyingi na namba mbili darasani akaipoteza
na kifupi sina cha kueleza yupo vipi sasa hivi.
Zinavyosema Tafiti.
Wanasaikolojia chanya “Postive Psychology” katika tafiti
wanaelezea Kuridhika
au kuwa na shukrani ni hali ya kihisia ya kukubali kile ambacho umejaliwa nacho
au unacho “moyo wa shukrani”, kinyume na hali ya “nataka-nataka” wakati wote
hivyo.
Tafiti
bado zinaeleza tunaweza stawisha tabia ya kuridhika na kusaidia kuongeza ubora
wetu katika kuyafurahia maisha.
Pia
hali ya kuridhika au kuwa na moyo wa shukrani hinausishwa sana katika kuwa na
nguvu mitazamo chanya “Optimism” na kuchukuliana na wanadamu wengine.
2.
TABIA
YA UKARIMU NA KUJITOA KWA WENYE UHITAJI.
Hiki ni mojawapo ya maswali ambayo yaliulizwa katika
utafiti uliotoa ripoti ya taifa la Finland kama watu wenye furaha duniani.
Katika tafiti hiyo kulikuwa na swali je humeweza kutoa msaada wowote kwa
wahitaji kwa mwezi uliopita?.
(Hakuna tatizo katika kumiliki mali nyingi maishani lakini
hakukufanyi kujitosheleza na kila kitu kiini cha utoshelevu ni alama gani nyuma umeacha kwa jamii yako.)
Hapo zamani kidogo kabla sijapata uelewa mara
inapotokea kijana anatangulia mbele za haki kwa ghafla mimi huwa ninawahi
kuuliza “hivi hajaacha hata mtoto” huku nikisikitika lakini hapo awali sikujua
motisha ya swali hili ndani yangu sababu baadae nikagundua watu wengi huuliza
hivyo pia.
Unapozungumzia Mwili kumbuka hata wanyama wana miili
unapozungumzia roho kumbuka hata wanyama wana roho lakini motisha ya utu wa
ndani kwa kundi lote hili ni kuacha vizazi vyetu vikiendelea kuwepo na ndio
sababu wengi sana wanaumizwa na suala la ugumba sababu kanuni iliyo ndani ya
utu wetu ni kinyume na kutoweka “extinction”. Hii imesaidia sana binadamu
tuendelee kuwepo na pia wanyama.
Lakini haitoshi tunaweza kusema kwa kigezo hicho tu
ni cha chini sana katika kutuhakikishia “ku survive” kwetu sababu kuna kitu
tumewazidi wanyama na hicho ni nafsi (ndani ya nafsi kuna Utashi,Akili na
hisia) wanyama hawana nafsi wana roho tu.
Hivyo matendo yote yenye ukarimu na misaada kwa
ndugu na jamii inayotuzunguka pasipo mipaka ya sheria, tamaduni, taratibu
na imani zetu ikiwa ina msingi wa utu na
upendo wa kuwajari wengine ni sababu kubwa sana ya furaha maishani kwetu
usipuuzie hili.
(Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi
elezea namna alivyojisikia “fahari” siku alivyopewa nafasi kwa utambulisho wa
heshima katika mazishi ya Nelson Mandela (yaliyotazamwa kwa Televisheni karibu
ulimwenguni pote). Kutokana na alama “the
legacy” aliyoiacha muhasisi wa taifa letu Hayati Mwalimu Nyerere kwa nchi
za kusini mwa Afrika, wakati wa harakati za ukombozi dhidi ya ubaguzi wa rangi
na ukoloni. Swali Ni namna gani?
ulijisikia kuwa Mtanzania siku hiyo <jibu (1)Huzuni au (2)Furaha>).
Kama ulijisikia furaha sana na ufahari kwa mema
aliyoyafanya mtu mmoja akiwakilisha taifa zima la watanzania je kwanini na wewe
usianze leo kutenda mema na maadili kwa watu waliokuzunguka.
Katika saikolojia
kuacha alama “legacy” ni inaeleweka kama nini ntakacho acha nyuma baada ya kufa
au ni kumbukumbu zipi nawaachia wanadamu wenzangu baada ya kufa na wanatambua
moja ya sababu ya kutafuta kusudi katika maisha ni kumbukumbu utakayoiacha
baada ya kundoka katika ulimwengu huu.
3.
KUTUMIA
KIPAWA “GIFTEDNESS” AU KARAMA YAKO.
(Tafiti zinadhibitisha kufanya kazi (zinazohusisha
kutumia vipawa vyetu) zinasaidia kutupa furaha na mafanikio katika maisha)
Kipawa maana yake ni nini? Ni uwezo wa kuzaliwa wa
kumwezesha mtu kufanya jambo Fulani. (Kamusi ya karne ya 21, 2011).
Kwa lugha ya
kiingereza kipawa ni “talent”,
“gift”, “ability”.
Kama ni msomaji wa makala hii ni ambaye ni Mama
(Mzazi) tayari. Wakati hupo labor kujifungua. Je wangapi unawakumbuka?.
Katika watu waliokuhudumia siku hiyo najua huwezi msahau Nesi aliyekuonesha
upendo na kukufariji au daktari aliyekuhudumia kwa upendo siku hiyo.
Kama ni mwanafunzi wa ngazi yoyote kuanzia sekondari
hadi chuoni najua huwezi msahau mwalimu aliyejitoa kwako kwa upendo katika
kukufundisha.
Mimi binafsi
huwa simsahau mwalimu wangu Mr Ali (Kwa sasa ni mkufunzi chuo kikuu huria “Open
University of Tanzania” ) kwa namna alijitoa wakati tupo sekondari hadi
kutufuata kule tulipoishi na wenzangu(wakati huo tulipaita “ghetoni”)
kutufundisha bila kumlipa chochote kile. na pia muda aliyojitolea wa ziada
shuleni kutufundisha masomo ya sanaa darasani nje ya ratiba ya shuleni. Na pia
siku hile tulivyofurahia wote matokeo yangu ya kidato cha nne ijapokuwa
yalikuwa ya wastani tu lakini alinitia moyo katika safari yangu kwenda vidato
vya juu.
Labda ni nini motisha ya ya Daktari, Nesi, Mwalimu
au mfanyabishara anayekuhudumia vizuri kwa ukarimu mara unapofika dukani kwake?.
Na kwanini kila mtu katika kumbukumbu zake anamuelezea vizuri tu kama wewe
unavyomuelezea?.
(“..Kipawa ni “kama kito cha thamani”
machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa...” Mithali 17:8)
Kuna vitu tunazaliwa navyo kuna ujuzi kipawa karama
tunazaliwa navyo kila mmoja ana cha kwake pale tunapoviendeleza au kuvitumia na
kugusa jamii zetu kwa namna moja au nyingine kunatupa kufanya kazi pasipo
kuchoka wala kutaka kupewa “over time” sababu ndani ya kukufanyika kazi kipawa
hicho hipo kufurahia maisha na pasipo tunaowahudumia kujua hilo na wao wanatufurahia
wakiita majina ya “ukarimu” na “upendo” pasipo kujua msingi wa furaha nikutumia
vipawa vyetu.
Maswali
Je ninaweza fahamu vipi kipawa changu nilichopewa?
Kwanini kazi ninayoifanya inanichosha sana na sina furaha nayo?
Je kinachokufanya uendelee kubaki katika kazi hiyo ni mshahara
tu au sababu hauna uamuzi mwingine “other option”?
(makala
hii yakuhusu “kipawa” tu naendelea kuiandaa na itakusaidia kufahamu vipawa
vyako vilivyopo katika ufahamu wa ndani “Unconscious” kama haujatambua bado)
Maoni
Chapisha Maoni