Mbinu za Kukusaidia kuishi kwa Furaha maishani

SABABU ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUKUJENGA NA KUYAFURAHIA MAISHA. Katika sehemu ya kwanza niliangazia sana “baadhi tu” ya maeneo ambayo tunakuwa tunayatarajia sana kama ndio sababu kuu sana kuja kutupa maisha mazuri na yenye furaha. Na nikitoa mifano halisi na tafiti mbalimbali ambazo zimewahi kufanyika ulimwenguni kote hasa kuhusu vipengele au vipaumbele ambavyo tumeviweka maishani kwetu kama sababu ya kutufanya tuwe na furaha lakini sio. (Hakuna kitu nimefundisha na kukiandika kama hakina ushahidi wa kitafiti kutoka kwa wanasaikolojia na wanasayansi) Basi katika sehemu hii ya pili pia nimeangazia tabia au matendo na mwenendo ambao unaweza kukusaidia kuwa na maisha yenye furaha kama ukusoma sehemu ya kwanza jitahidi upitie ili hiwe na rahisi kwenda pamoja nikirejea ripoti ya taifa la Finland mshindi wa mwaka 2018 kama taifa la watu wenye furaha duniani. Pia ili huweze kufuatilia vizuri mafundisho haya kuhusu Saikolojia na maisha ni vizuri kama utaanza ni follow katika ...